Lula da Silva kufunguliwa mashtaka

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa zamani Luiz Inacio Lula da Silva

Viongozi wa mashtaka nchini Brazil wanasema kuwa watamfungulia mashtaka ya kujipatia fedha kwa njia haramu aliyekuwa rais wa taifa hilo, Luiz Inacio Lula da Silva.

Wanasema kuwa bwana Lula pamoja na mkewe walishindwa kutangaza umiliki wao wa nyumba moja ya kifahari kwenye ufuo wa bahari katika eneo la Guaruja.

Rais huyo wa zamani ambaye ni mashuhuri kwa sasa nchini Brazil amekanusha madai hayo aklisema kuw ayamechochewa kisaia.

Nyumba hiyo inamilikiwa na kampuni moja ya ujenzi ambayo imehusishwa na sakata moja kubwa katika kampuni ya mafuta ya seriklai ya Petrobras.