Nchi tatu zapinga mapendekezo ya adhabu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption vikosi vya kijeshi

Nchi za Urusi,Misri na Senegal zimepinga mapendekezo ya adhabu ya kurejeshwa nyumbani kwa kikosi kizima cha kulinda amani iwapo itabainika askari kufanya ukatili wa kingono. Badala yake wametaka adhabu hiyo kuwalenga askari watakaobainika tu.

Umoja wa mataifa umetoa mapendekezo hayo kwa lengo la kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya walinzi wa vikosi vya kulinda amani amani dhidi ya watoto.

Mapendekezo hayo yanaungwa mkono na katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Ban Ki-Moon ambaye ameliambia baraza la usalama kutilia mkazo jambo hilo.

Adhabu hiyo imetajwa kuwa itatakiwa kumlenga mhusika tu na si kikosi chote.