5 wauawa kwa kupigwa risasi Marekani

Image caption Watu 5 wauawa katika mji wa Pittsburg, Marekani.

Takriban watu watano wameuawa wakati wa ufyatuaji wa risasi karibu na mji wa Pittsburg ulio kwneye jimbo la Pennsylvania.

Maafisa wanasema kwa watu waliokuwa na silaha walifyatua rais kwenye sherehe moja ambapo pia watu wengine watatau walijeruhiwa.

Wanne kati ya wale waliouawa walikuwa ni wanawake huku watu waliofanya mauaji hayo wakiwa bado hawajakamatwa.

Misururu ya mauaji kwa kutumia bunduki yamechangia suala la umiliki wa bunduki kuwa mjadala mkubwa nchini Marekani.

Watu wanne walikufa eneo la mkasa huku mmoja akiaga dunia alipokufikishwa hospitalini. Wanaume wawili waliojeruhiwa wako katika hali mahututi.