Ben Carson amuunga mkono Donald Trump

Image caption Carson na Trump

Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican Ben Carson amethibitisha kwamba anamuunga mkono aliyekuwa mpinzani wake Donald Trump katika kinyang'anyiro cha urais nchini Marekani.

Carson alimuidhinisha katika mkutano wa pamoja na wanahabari mjini Florida huku Trump akiwa anaongoza katika kura ya mchujo wa kumtafuta atakayewania urais kupitia chama hicho kabla ya Jumanne kuu.

Bwana Carson ,aliye kifua mbele aling'atuka wiki iliopita baada ya kushindwa kuungwa mkono.

Ni mgombea wa pili kumuidhinisha bwana Trump baada ya Gavana wa jimbo la New Jersy Chris Christie.