Nyota wa Home and Away ashtakiwa kwa ubakaji

Image caption Nyota Martin Lynes

Aliyekuwa msanii wa kipindi cha Home and Away ameshtakiwa na ubakaji pamoja na kumshambulia mwanamke.

Martin Lynes mwenye umri wa miaka 48 anatuhumiwa kwa kumshambulia mwanamke mwenye umri wa miaka 51,nyumbani kwake News South Wales Central Coast.

Bwana Lynes ameliambia gazeti la The daily Telegraph kwamba amekuwa akipinga shtaka hilo na kwamba atayakabili mashtaka hayo.

Akiwa mfanyikazi wa kampuni ya kuuza nyumba,Lynes alikuwa maarufu katika kipindi cha Australia cha Home and Away akiigiza kama muhalifu Adam Sharpe.

Pia aliigiza katika filamu ya All saints kama Luke Forlano.

Amewachiliwa kwa dhamana ya masharti na kuagizwa kufika mahakamani tarehe 27 Aprili.