Welby:Walio na hofu ya wahamiaji sio wabaguzi

Haki miliki ya picha PA
Image caption Askofu mkuu Justin Welby

Askofu mkuu wa kanisa la Cantebury Justin Welby amesema kuwa ni makosa kuwataja watu walio na wasiwasi kuhusu uhamiaji kuwa wabaguzi.

Kuna wasiwasi kuhusu athari za nyumba za kuishi ,kazi na afya,aliliambia bunge.

Hatahivyo aliitaka Uingereza kuchukua baadhi ya wahamiaji na wakimbizi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji

Bwana Welby pia alitaka kufanyika kwa mjadala ulio na maono kuhusu kura ya maoni na kusema kuwa hakuna mkristo yeyote aliye na maoni ya sawa kuhusu vile Waingereza wanapaswa kupiga kura.

Amesema:Lazima tujiamulie lakini pia lazima tujue tunafanya nini duniani.Taifa hili lina historia ya kipekee tukiangazia miaka 100 iliopita.