Newcastle yampiga kalamu kocha wake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption McClaren

Kilabu ya Uingereza ya Newcastle imemfuta kazi mkufunzi wake Steve McClaren.

Kocha huyo wa zamani wa Uingereza alishinda mechi sita kati ya 28 katika kilabu hiyo ambayo inakaribia kushushwa daraja katika ligi hiyo.

McClaren na timu yake walizomwa baada ya kushindwa 3-1 na kilabu ya Bournemouth katika uwanja wa nyumbani wa St James Park ikiwa ni mara yao ya tatu kushindwa.

Aliyekuwa kocha wa Liverpool,Chelsea,Real Madrid na Intermilan, Rafael Benitez huenda akachukua mahala pake.

McClaren alitia saini kandarasi ya miaka mitatu na Newcastle mnamo mwezi Juni baada ya kilabu hiyo kuzuia kushushwa daraja katika siku ya mwisho msimu uliopita.