Washambuliaji wa Paris wapatikana katika faili za IS

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Faili za Islamic State

Majina ya washambuliaji watatu wa kujitolea muhanga mjini Paris yamepatikana katika faili za siri zilizopatikana kutoka kwa kundi la Islamic State,kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Watatu hao wanaaminika kutekeleza shambulio baya zaidi katika ukumbi wa Bataclan ambapo watu 90 walifariki.

Faili hizo za IS zilizopatikana na polisi wa Ujerumani ,Uingereza na vyombo vya habari nchini Syria zimedaiwa kuwatambua maelfu ya wapiganaji wa Jihad kutoka takriban mataifa 40.

Maafsa wa Ujerumani wamesema kuwa faili hizo huenda ni za ukweli.

Image caption Wapiganaji wa IS wanaosakwa

Takriban wapiganaji 22,000 wameripotiwa kugundiliwa na stakhabadhi hizo,huku faili moja ya walioajiriwa ikiwa na jina kule anakoishi na habari nyengine.

Hatahivyo majina mengi yaliopatikana yemefanana.