Shambulio la Israel lamuuwa mvulana Mpalestina

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Palestina

Maafisa wa afya katika utawala wa Palestina wanasema kuwa mvulana mmoja wa umri wa miaka kumi ameuwawa na mashambulizi ya angani ya Israeli kaskazini mwa Ukanda wa Gaza huku ndugu zake wawili wakijeruhiwa.

Jeshi la Israeli lilisema kuwa lililenga ngome mbili za Hamas kujibu mashambulizi ya roketi yaliyofaywa dhidi ya Israeli.

Lilisema kuwa takriban makombora manne yaliyofyatuliwa kutoka ukanda wa Gaza yalianguka eneo lililo wazi karibu na mji wa Israeli wa Sderot.