Manuwari ya Korea Kaskazini yatoweka

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Kim Jong un

Ripoti zinasema kuwa Korea Kaskazini inatafuta moja ya manowari yake baada ya kupoteza mawasiliano nayo mapema wiki hiii.

Manowari hiyo ilikuwa ikuhudumu nje ya pwani ya Korea Kaskazini kwa siku kadhaa wakati ilipotoweka.

Ajali hiyo inajiri wakati kuna hali ya wasi wasi katika eneo hilo wakati Korea Kusini na Marekani wanaendelea na mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi kuwahi kushuhudiwa.

Korea Kaskazini imetoa tisho lingne la vita kutokan na mazoezi ya kijeshi yanayofanywa na vikosi vya Marekani na Korea Kusini.

Jeshi la Korea Kaskazini lilisema kwa liko tayari kufanya mashambulizi ikiwa kuna dalili ya maandalizi ya kufanya uvamizi dhidi yake.

Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitishia kuendesha vita vya kunukilia kujibu mazoezi hayo ya pamoja ambayo marekani na korea kusini zinasema ni ya kujilinda na pia ya kawaida.