Rwanda yapuuza madai ya ujasusi ya Burundi

Image caption Rwanda yapuuza madai ya ujasusi ya Burundi

Rwanda imekanusha madai ya Burundi kwamba mtu aliyekematwa mpakani Burundi alikuwa jasusi wake.

Shirika la habari la Reuters liliripoti wakuu wa Burundi wakidai kuwa mtu huyo ni mwanajeshi wa Rwanda aliyetumwa Burundi kuleta vurugu.

Na shirika la AFP linaarifu kuwa Rwanda limetoa maanani tuhuma hizo za Burundi kuwa ni za upuuzi, na kwamba kufuatana na jina, hawakuwa na mtu huyo katika jeshi la Rwanda.

Wakuu nchini Burundi kwa upande wao wamemtoa mtu mmoja Rucyahintare Cyprien mbele ya wanahabari wakisema ni jasusi wa Rwanda.

Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita hata hivyo amekanusha madai hayo.

Image caption Kufikia sasa takriban watu 400 wameuawa huku zaidi ya lakini mbili u nusu wakitorokea mataifa jirani.

''Hayo majina hayapo kabisa katika kumbukumbu zote za Burundib (jeshi la Rwanda)'' Kwa upande wake msemaji wa polisi wa Burundi Pierre Nkurikiye mtuhumiwa huyo ametekeleza operesheni tatu nchini Burundi kwa nia ya kutibua machafuko nchini humo.

Uhusiano baina ya mataifa hayo mawili jirani uliharibika baada ya madai ya Burundi kuwa jirani wao Rwanda ndio wanaochochea machafuko nchini humo kuungwa mkono na ripoti moja ya Umoja wa mataifa.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Burundi imekumbwa na machafuko ya kisiasa tangu rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wake wa tatu

Burundi imekumbwa na machafuko ya kisiasa tangu rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania muhula wake wa tatu mwezi Apili mwaka uliopita.

Wapinzani wake wanadai alikiuka katiba huku mwenyewe akishikilia kuwa muhula wake wa kwanza hakuchaguliwa na wananchi.

Kufikia sasa takriban watu 400 wameuawa huku zaidi ya lakini mbili u nusu wakitorokea mataifa jirani.