Wafungwa wa ngono wa IS wazuiwa kushika mimba

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kundi la IS, limekiri kuwatumia wanawake hao kama watumwa kingono

Uchunguzi uliofanywa na gazeti la New York Times, umetambua kuwa kundi la wapiganaji la Islamic State, linalowashikilia wanawake kutoka jamii ya Yazidi sasa linawapa wafungwa hao wa ngono vifaa vya kuwazuia kushika mimba-- ili kuendelea kutumika na wanamgambo hao.

Gazeti hilo lililowahoji zaidi ya wanawake 35 kutoka kwa jamii hiyo ndogo ya Yazidi, waliokimbia maafa ya wanamgambo wenye itikadi kali nchini Iraq linasema kuwa dawa za kupanga uzazi za kumeza pamoja na za kudungwa zimekuwa zikitumika.

Image caption Wafungwa wa ngono wa IS wazuiwa kushika mimba

Aidha, ripoti za wanawake kuavya mimba pia ziliripotiwa.

Kundi la IS, limekiri kuwatumia wanawake hao kama watumwa kingono.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la IS, limekiri kuwatumia wanawake hao kama watumwa kingono.

Kumekuwa na madai ya ubakaji wa wanawake na wasichana wa Yazidi kwa muda mrefu, huku wakitumia dhana wanayosema kuwa, unaweza kumbaka mwanamke mradi hashiki mimba.