Afrika Kusini yapoteza kesi ya Bashir

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Sudan Omar el Bashir akishuka kutoka katika ndege

Serikali ya Sudan Kusini imefeli kubatilisha uamuzi wa mahakama unaoishtumu kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omal al- Bashir wakati alipohudhuria mkutano wa AU mnamno mwezi juni.

Kushindwa kwa serikali kutekeleza agizo la kumkamata lililotolewa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC ni kinyume na sheria za taifa hilo,mahakama ya rufaa iliamuru.

Mahakama ya chini ilitoa uamuzi kama huo,na serikali ina matumaini kwamba itashinda rufaa.

Inahoji kwamba Bashir ana haki ya kinga ya kirais.