Lula da Silva sasa kuwa waziri Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa rais wa Brazil Lula da Silva

Aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Luis Inacio Lula da Silva, amekubali cheo cha uwaziri ndani ya serikali ya Dilma Rousseff.

Wanachama wa chama cha wafanyikazi wamesema kuwa uteuzi huo utaupa nguvu utawala wake unaolegea.Akiwa waziri Lula atakuwa na haki ya kinga.

Wiki iliopita waendesha mashtaka walitaka akamatwe kutokana na uchunguzi wa ulanguzi wa fedha wa jumba moja la kifahari lililopo katika ufukwe wa bahari.

Rais huyo wa zamani aliye na umaarufu mkubwa amekana kufanya makosa yoyote na kusema kuwa madai hayo yanashinikizwa kisiasa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jumba la kifahari linalodaiwa kumilikiwa na Lula da Silva

Akiwa waziri Lula anawezi kushtakiwa na mahakama ya juu pekee na hivyobasi kumuondoa mbele ya meno ya jaji aliye kusini mwa mji wa Curitiba ambaye anahusishwa na uchunguzi huo.

Lula alizuiliwa kwa mda mapema mwezi huu baada ya uchunguzi kusema kuwa kuna ushahidi alipokea faida katika mpango ulioshirikisha kampuni ya mafuta ya Petrobras.