Mwanasiasa ashtakiwa kwa kumpiga farasi India

Image caption Farasi India

Maafisa wa polisi nchini India wameanzisha kesi dhidi ya mwanasiasa kutoka chama tawala cha BJP aliyedaiwa kumshambulia farasi mmoja wa polisi wakati wa maandamano katika jimbo la kaskani la Uttarakhand.

Ganesh Joshi,mbunge wa mji wa mlima wa Mussoories amedaiwa kumpiga mnyama huyo na fimbo.

Farasi huyo anayejulikana kama Shaktimaan,alipata majeraha mabaya na ripoti nyengine zimesema kuwa atahitaji kukatwa mguu.

Bwana Joshi amesema kuwa mashtaka dhidi yake yameshinikizwa kisiasa.

''Kanda ya video inayonionyesha nikibeba fimbo mbele ya farasi huyo haina uhusiano wowote na kanda ya video nyengine iliopigwa zamani nikibeba fimbo mbele ya farasi huyo '',joshi aliiambia BBC.

''Farasi huyo alianguka baada ya mtu kuvuta kiti kilichokuwepo juu yake na kupata jereha la mguu'',aliongezea.

Kisa hicho kilitokea karibu na bunge katika mji mkuu wa jimbo hilo Dehradun siku ya Jumatatu wakati BJP ilipokuwa ikiandaa maandamano dhidi ya chama tawala cha Congress.