Picha ya utupu wa Kim Kardashian yafutwa Australia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kanye West na mkewe Kim Kardashian

Picha iliochorwa ya utupu wa Kim Kardashian imefutwa siku chache tu baada kuchorwa na msanii mmoja mjini Melbourne nchini Australia.

Picha hiyo ilichorwa na msanii Lush Sux katika ukuta mmoja wa makaazi ya mji huo.

Lakini picha hiyo yenye urefu wa mita 10 ilirushiwa rangi mbali na kuwekewa maandishi machafu yalioandikwa chini yake.

Lush Sux ambaye jina lake ni Mark Walls aliwaambia wapita njia kwamba alikasirishwa kuona kuwa mchoro huo umemwagiwa rangi.

Image caption Picha ya utupu wa Kim Kardashian iliofutwa

''Niliona umuhimu wa kuichora picha hii mara moja nilipoiona katika mtandao wake wa Instagram hadharani,katika jengo moja la ghorofa tatu''.

''Pengine pia mimi hupenda kuangaziwa kama yeye''.Picha hiyo ilichorwa katika ubavu wa ukuta mmoja unaomilikiwa na kampuni ya uchoraji ya Melbourne.

Ukuta mwegine uliopo mkabala na picha iliomwagiwa rangi una picha ya mgombea wa urais wa Marekani Donald Trump.

Kim Kardashian alikosolewa kwa kuweka picha hiyo ya utupu katika mtandao wa instagram katika siku ya kimataifa ya wanawake .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kim Kardashian na Kanye West

Aliwashtumu wakosoaji wake akisema imetosha kwa kuuaibisha mwili wake.

Aliwaambia mashabiki katika mtandao wake :''Mimi ni mama,mimi ni mke wa mtu,mimi ni dada na mtoto wa mtu,mfanyibiashara na ni haki yangu kuwa na umbo la kuvutia.Mwili wangu umenipa fursa hiyo,na jinsia yangu.Nimepewa fursa ya kuuonyesha ulimwengu kuhusu nilivyo na siogopi kile mtu yeyote atakachosema.Nachukua fursa hii kuwashinikiza wasichana na wanawake duniani kufuata nyayo zangu''.