Walipuliwa wakiwa katika ibada Nigeria

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko uliotokea katika msikiti wa Nigeria hapo awali

Mlipuaji wa kujitoa mhanga amewaua waumini 22 katika msikiti mmoja kando kando ya mji wa Kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria kulingana na chombo cha habari cha AP.

Mlipuaji wa kwanza alijilipua ndani ya msikiti huku wa pili akijilipua nje huku walionusurika wakijaribu kutoroka walioshuhudia waliambia BBC.Watu wengine 17 walijeruhiwa katika shambulio hilo afisa mmoja wa AFP amesema.

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekuwa wakiulenga mji huo katika mashambulio yao ya miaka 17.

''Tulikuwa mita chache kutoka katika msikiti huo wakati tuliposikia sauti kubwa na kile kilichofuatia ni moshi mkubwa na mili iliokuwa imetapakaa kila mahali,shahidi mwengine alikimbia kituo cha habari cha AP.

Shambulo hilo lilifanyika dakika chache tu baada ya waumini kuanza ibada ya alfajiri ,imam mkuu wa Umarari Mosque aliambia BBC.

Wote waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini,aliongezea