Wapenzi wa jinsia moja washinda kesi Botswana

Image caption Mapenzi ya jinsia moja

Mahakama ya juu nchini Botswana imekataa jaribio la serikali kuvunjilia mbali kundi la wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja katika ushindi usio wa kawaida kwa wanaopigania haki za watu hao barani Afrika.

Kulingana na shirika la habari la reuters mahakama ya rufaa ilikubali uamuzi wa mahakama ndogo wa mwaka 2014 kwamba wapenzi wa jinsia moja kutoka kundi la LEGAGIBO nchini Botswana wakubaliwe kujisajili na wapiganie mabadiliko katika sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

''Ni wazi kwamba uamuzi wa serikali wa kutaka marufuku hiyo itekelezwe inaingilia haki za mlalamishi kubuni muungano wa kutetea haki zake ili kukuza maslahi,''jaji Ian Kirby alisema.

Vitendo vya wapenzi wa jinsia moja ni haramu nchini Botswana.

Uamuzi huo umepongezwa na baadhi ya raia katika mtandao wa Twitter