Mwanamuziki mashuhuri Malawi afariki

Haki miliki ya picha Grace Chinga Facebook

Mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini Malawi Grace Chinga amefariki.

Rafiki wa karibu wa familia yake, Pasta Chris Suya, amenukuliwa na gazeti la gazeti la Nyasa Times la Malawi akisema mwanamuziki huyo alikimbizwa hospitalini baada ya kulalamikia maumivu makali ya kichwa.

"Tulipokea simu kwamba alikuwa anatatizwa na maumivu ya kichwa na tukakimbia kwake nyumbani mwendo wa saa moja jioni. Tulimpeleka hospitali ya Queens Elizabeth ambapo, alifariki.”

Kwa mujibu wa ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook, mwanamuziki huyo alikuwa akijiandaa kuchomoa albamu mpya.

Raia wa Malawi wamekuwa wakituma salamu za rambirambi kwenye mitandao ya kijamii kumuomboleza.