Islamic State wametekeleza ‘mauaji ya halaiki’

IS Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kundi la Islamic State linadhibiti baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati

Marekani imesema kundi la wapiganaji wa Kiislamu linalojiita Islamic State (IS) limetekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Wayazidi, Wakristo na waislamu wa madhehebu ya Shia.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry ametangaza IS, kundi ambalo limekuwa pia likiitwa Daesh, kuwa la “mauaji ya halaiki kwa kujitangaza kwenyewe, sera na matendo”.

Bw Kerry pia amesema kundi hilo limtekeleza makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari.

Amesema Marekani imefikia uamuzi huo kwa kufuata habari ambazo zimekusanywa na vyanzo mbalimbali.