Korea Kaskazini yarusha makombora 2 baharini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Korea Kaskazini yarusha makombora mawili baharini

Taifa la Korea Kaskazini limerusha makombora mawili ya masafa marefu katika bahari ya mashariki ya pwani yake,siku chache baada ya kiongozi wake Kim Jong-un kuagiza majaribio ya mabomu zaidi ya kinuklia na silaha nyengine.

Marekani imejibu kwa kutoa wito kwa Pyongyang kutozua wasiwasi katika eneo hilo ambao umekua juu tangu Korea Kaskazini kufanya jaribio la nne la mabomu yake ya kinyuklia mnamo mwezi Januari.

Korea Kusini imeelezea jaribio hilo la hivi karibuni kama tishio kubwa la usalama na udhabiti wa eneo hilo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Korea Kaskazini

Shirika la habari la Korea Kusini Yonhap limesema kuwa kombora la pili huenda liliharibika hewani.

Ripoti za awali zilisema kuhusu kombora moja lililorushwa.