Musharraf aruhusiwa kupata matibabu Dubai

Image caption Pervez Musharraf

Aliyekuwa kiongozi wa kijeshi nchini Pakistan Pervez Musharaf amewasili mjini Dubai kupata matibabu baada ya serikali kumuondolea marufuku ya usafiri aliyowekewa mwaka 2013.

Bwana Musharaf anakabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo uhaini wa kukiuka katiba na kutangaza hali ya hatari mwaka 2007.

Aliondoka madarakani mwaka mmoja baada ya utawala wake kukabilia na upinzani mkali.

Mwandishi wa BBC anasema kuwa kuondolewa kwa vikwazo hivyo ni kama pigo kwa waziri mkuu Naawaz Sharif ambaye aliahidi kumuwajibisha Musharraf kutokana na vitendo vyake vilivyokuwa kinyume na sheria.