Raia wa Congo kumchagua rais mpya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Congo akishiriki uchaguzi uliopita

Wakuu katika serikali ya Jamhuri ya Congo wameamrisha kampuni mbili kuu za simu, kufunga mawasiliano yote ya simu, wakati wa uchaguzi wa urais hapo kesho.

Wizara ya mashauri ya ndani ya nchi ilisema imefunga mawasiliano kwa sababu za usalama.

Mgombea wa upinzani, John Marie Michel Mokoko, alisema amepokea amri ya kwenda polisi, na alisema hiyo ni hatua ya kumzuia yeye katika kugombea uchaguzi.

Wagombea wanane wanampinga Rais Denis Sassou Nguesso.

Katiba ilibadilishwa mwaka jana, kumruhusu agombee tena uongozi.