Mshukiwa mkuu wa shambulio la Paris akamatwa

Haki miliki ya picha EVN
Image caption Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji wakimkamata mshukiwa

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameonya kuwa mitandao ya kigaidi barani Ulaya inaendelea kuimarika licha ya kukamatwa kwa mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya mwezi Novemba mjini Paris.

Salah Abdeslam alikamatwa wakati wa uvamizi uliofanywa na kikosi cha kupambana na ugaidi nchini Ubelgiji katika wilaya ya Molenbeek mjini Brussels baada ya kupigwa risasi kwenye mguu.

Haki miliki ya picha
Image caption Eneo lililovamiwa na maafis wa polisi

Mtu mwingine ambaye pia anashukiwa kuhusika kwenye mashambulizi hayo ya mwezi Novemba alijeruhiwa na kukamatwa na kwa ujumla watu watano walikamatwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa polisi

Bwana Hollande alisema kuwa vita havitakwisha hadi kila mmoja aliyehusika kwenye shambulizi la Paris akamatwe. Watu 130 waliuawa wakati wa shambulizi hilo.