Mshukiwa wa Paris aruhusiwa kutoka hospitali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Abdesalam

Mshukiwa mkuu wa mashambulio ya mjini Paris, Salah Abdeslam, ameruhusiwa kutoka hospitali na kuwekwa kizuizini na polisi nchini Ubelgiji, baada ya kujeruhiwa katika operesheni ya polisi ambapo alikamatwa.

Rais Francois Hollande wa Ufaransa, anasema anataraji kuwa Abdeslam atapelekwa Ufaransa katika siku chache zijazo.

Idara ya usalama inataraji kuwa ataweza kutoa habari kuhusu njama nyengine, na mitandao inayohusika na kundi la Islamic State katika bara la Ulaya, na pengine afichue nani alihusika na kupanga na kugharimia mashambulio ya mjini Paris.

Watu mia moja na 30 waliuwawa katika mashambulio ya Paris mwezi Novemba.