Ndege yaanguka na kuwaua watu 62 Urusi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege ya Flydubai

Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 62 imeanguka ilipokuwa ikitua katika mji ulio kusini mwa Urusi wa Rostov-on-Don.

Hakukuwa na manusura kati ya abiria 55 na wahudumu saba waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikitoka Dubai ilimilikiwa na shirika la Fly Dubai.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege ya Flydubai ilioanguka nchini Urusi

Ndege hiyo ilizunguka angani kwa karibu masaa mawili kabla ya kufanya jaribio la pili la kutua kufuatia hali mbaya ya hewa.

Ilianguka mita mia kadha kutoka kwa barabara ya uwanja wa ndege ambapo ilivunjika na kushika moto.