Mtu asiyejulikana adai ''kumdukua'' Trump

Haki miliki ya picha
Image caption Trump

Wiki mbili zilizopita mtu ambaye hakutaja jina lake alitangaza vita dhidi ya mgombea aliyekifua mbele katika chama cha Republican Donald Trump.

Na sasa akaunti inayodai kuwakilisha kundi la mdukuzi huyo limetoa kile linasema ni habari binafsi za Trump pamoja na zile za faragha.

Udukuzi huo unashirikisha habari za siri ikiwemo nambari ya simu ya mgombea huyo pamoja na bima ya usalama na eneo analoishi,tarehe yake ya kuzaliwa na majina ya wazazi wake.

Tulijaribu kulikagua kundi hilo kwa kutafuta katika mtandao kwa saa moja.

Na hivi ndivyo tulivyobaini.

Kwamba tarehe ya kuzaliwa ya Donald Trump,wazazi wake,watoto,tarehe ya eneo la kuzaliwa iko katika mtandao wa Wikipedia.

Habari hiyo pia inashirikisha ukurasa wa Mar-a-lago ,Palm Beach mjini Florida ambayo ndio anwani ilioorodheshwa katika udukuzi huo.

Eneo anakoishi pia lilibainiwa na wadukuzi hao lakini makao yake pia yanapatikana wakati mtu anapoyasaka katika huduma ya ramani ya Google.