Vikosi vya Kenya na al-Shabab vyapigana

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Kenya wanasema waliwaua wanamgambo 21 wa al shabbab

Kumekuwa na mapigano kati ya wanajeshi wa kenya na wanamgambo wa al-Shabaab katika eneo la Lower Juba nchini Somalia.

Kuna ripoti za kukanganya kuhusu maafa.

Wanajeshi wa Kenya wanasema kuwa walivisiwa lakini wakafanikiwa kuwaua wanamgabo 21 licha ya wao kupoteza wanajeshi wawili.

Al-Shabab nao wanadai kuwa waliwaua wanajeshi 20 wa Kenya wakawakamata wawili na kuharibu magari yao sita.

Mapigano hayo yalitokea kwenye barabara inayoelekea mji wa Afmadow ambapo wanajeshi wa kenya waliwaua wanamgambo 19 wa al-Shabab siku ya Jumatano.