Maandamano yazuia mkutano wa Trump

Haki miliki ya picha Salim Rizvi
Image caption Waandamanaji wanaompinga Trump

Waandamanaji walifunga barabara katika jimbo la Arizona wakati Donald Trump alikuwa akijiandaa kufanya mkutano katika eneo la Phoenix.

Mgombea huyo mkuu wa kiti cha Republican kwenye uchaguzi wa urais nchini Marekani alihutubia wafuasi wake katika eneo la Fountain Hills.

Takriban waandamanaji 50 walisababisha kutokea kwa msongamano wa magari huku wakibeba mabango ya kumpinga Trump.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump alifanya mkutano wake katika eneo la Fountain Hills

Mikutano ya mfanyibiashara huyo tajiri imekumbwa ghasia siku za hivi majuzi. Mkutano wa Chicago wiki moja iliyopita ulifutwa baada ya kutokea kwa maandamano.

Mimia ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika katika jimbo la Illinois na mapigano kuzuka kati ya wafuasi na waandamanaji katika jukwa ambapo Trump alipanga kutoa hotuba yake.