Viongozi maarufu katika Twitter na Instagram

  • Huku mtandao wa Twitter ukiadhamisha miaka 10:Tunakuuliza je unadhani ni viongozi gani maarufu katika mitandao ya kijamii?.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption papa Francis

Mtandao wa Twitter umekuwa maarufu kwa maswala ya kisiasa miongoni mwa viongozi wa mataifa kadhaa pamoja na maafisa wa serikali.

Huku mtandao huo ukiadhimisha miaka 10 tunawaangazia viongozi mashuhuri ambao hawatoki katika mtandao huo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Taylor Swift

Wakati kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis alipoanzisha mtandao wake wa Instagram siku ya jumamosi ,alijiunga na nyota wa muziki Taylor Swift na Beyonce pamoja na mwanasoka Cristiano Ronaldo,akiwa miongoni mwa watumizi kumi bora wa Instagram duniani kutokana na idadi kubwa ya wafuasi aliopata.

Image caption Cristiano Ronaldo

Makao makuu ya kanisa katoliki The Vatican imethibitisha kuwa kiongozi huyo wa miaka 79 atakuwa katika mtandao huo wa picha chini ya jina Fransiscus.

Aliingia katika mtandao huo siku ya Jumamosi sanjari na maadhimisho yake ya tatu kama kiongozi wa kanisa katoliki.

Akiwa miongoni mwa watu maarufu katika mtandao huo,ni mpango wa hivi karibuni wa Vatican kuhakikisha kuwa Papa Francis ana ufuasi mkubwa.

Na si yeye pekee:Mitandao ya kijamii imeimarika na viongozi wengi duniani hujaribu kuitumia ili kuwafikia vijana wengi.

Ripoti ya ''Twiplomacy'' iliziangazia akaunti 700 za viongozi wa mataifa na serikali,mawaziri na maafisa katika mataifa 166.

Haki miliki ya picha PMO India
Image caption Narendra Modi na mfalme Salman wa Saudia

Baada ya Obama ,walibaini kwamba kiongozi maarufu zaidi ni waziri mkuu wa India Narendra Modi ,ambaye akaunti yake ilipata wafuasi wengi baada ya uchaguzi wa 2014.

Mnamo mwezi Machi alikuwa na wafuasi milioni 18.

Mimi naamini sana uwezo wa Teknolojia na mitandao ya kijamii kuwasiliana na watu.Aliandika katika ujumbe wake.

Image caption Tayyip Erdogan

Modi alimshinda rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan ambaye ni wa tatu lakini hajafikia hata nusu ya wafuasi wa kiongozi huyo wa India.

Umaarufu wa waziri mkuu wa India Narendra Modi pamoja na ufuasi mkubwa wa raia wa Uturuki pamoja na mfalme wa Saudia unaonyesha kwamba viongozi wa mataifa yenye idadi kubwa ya watu ambapo utumizi wa mtandao wa Twitter uko juu wana fursa kubwa ya kupata ufuasi mkubwa kulingana na Twiplomacy.

Mwanamfalme wa Saudia alipata umaarufu mkubwa katika akaunti yake baada ya kuidhinishwa kama Mfalme Salman mnamo mwezi Januari mwaka 2015.

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Rais Poroshenko wa Ukraine

Rais wa Ukraine Poroshenko alipata ufuasi mkubwa katika kipindi cha mwaka uliopita ,kufuatia makabiliano yake na Urusi.Miongoni mwa viongozi wa Ulaya hatahivyo yuko nyuma ya wengine wengi akiongozwa na waziri mkuu wa Uingereza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dilma Rousseff

Marekani Kusini ina viongozi wa Mexico Enrique Pena Nieto ambaye ana wafuasi milioni 5 akiwaongoza wenzake wa Colombia Juan Manuel Santos,rais wa Brazil Dilma Rousseff pamoja na rais wa Argentina Cristina Fernandez.

Rais wa Venezuela Nicholas Maduro na kiongozi mpya wa Argentina Mauricio Macri ni watano wakiwa na idadi sawa ya ufuasi.

Huku Maduro akiwa na akaunti ya kisiasa anayoitumia kuchapisha ujumbe 65 kwa siku mwaka 2015.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Paul Kagame wa Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta wamekuwa marais walio na ufuasi mkubwa barani Afrika wakiwa na wafuasi milioni 1.3 kila mmoja.

Haki miliki ya picha PSCU Kenya
Image caption Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya

Rais huyo wa Rwanda pia anajivunia rekodi nyengine:ni kiongozi anayezungumza sana katika mtandao wake wa Tweeter duniani akiwa na asilimia 86 ya majibu kwa wanaozungumza naye wakiwemo wakosoaji wake pamoja na watoto wake.

Ijapokuwa idadi aliyonayo iko chini kiasi ya ile ya viongozi wengine wa dini duniani ,Dalai Lama ana wafuasi milioni 12,licha ya kutuma ujumbe 1,100 katika miaka minane ya mitandao ya kijamii.

  • Instagram
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Barack Obama

Katika mtandao wa instagram rais wa Marekani Barack Obama anaongoza kwa umaarufu licha ya kwamba pia yuko katika tweeter na wafuasi milioni 6.6.

Alijiunga na siasa mwaka 2012.Lakini mwaka 2014 ripoti moja ya kidijitali ya Arc 3 ilionyesha kuwa picha 10 za kisiasa zilizopendwa katika mtandao wa Instagram pia zilisambazwa na Obama.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Urusi Medvedev

Katika nafasi ya pili ni waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev,aliye na mpiga picha ambaye humpiga picha kiongozio huyo na kuzituma mara moja kwa wafuasi wa kiongozi huyo.Narendra Modi ni watatu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Donald Trump

Na sio bahati nzuri kwamba Jarida la Times Magazine wiki hii lilimtaja kiongozi huyo wa taifa la India kama nyota wa mtandao mbali na kuwa miongoni mwa watu 30 walio na ushawishi mkubwa katika mtandao katika orodha ambayo pia inamuorodhesha mwanasiasa mmoja pekee Donald Trump.

Haki miliki ya picha
Image caption Ali Khamenei

Malkia Rania wa Jordan ameongeza ufuasi hadi milioni 1.5 baada ya kuchapisha ''kama mke aliye na kazi nzuri sana'',Amir wa Dubai ,Erdogan wa Uturuki,kiongozi wa kidini nchini Iran Ali Khamenei,rais wa Argentina Mauricio Macri na rais wa Misri el Sisi wanakamilisha kumi bora.