FBI huenda wakafungua simu ya muuaji

Farook Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Syed Farook aliwapiga risasi watu San Bernardino

Idara ya Haki ya Marekani imesema huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya kufungua simu ya mkononi ya muuaji aliyewapiga risasi watu eneo la San Bernardino, Syed Rizwan Farook.

Idara hiyo imeiomba mahakama kuahirisha kusikilizwa kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya utengenezaji wa simu, Apple.

Haki miliki ya picha epa
Image caption Simu ya iPhone

Idara hiyo imekuwa ikishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo la California, Desemba, mwaka jana.