Guardiola hawezi kujiondoa Manchester City

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pep Guardiola

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola atakuwa kocha wa timu hiyo msimu ujao hata iwapo timu hiyo haitafuzu kwa kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Kocha huyo wa Bayern Munich ametia kandarasi ya miaka mitatu kumrithi Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu huu.

Kushindwa kwa timu hiyo na kilabu ya Manchester United umeyaweka matumaini ya City kufuzu katika kombe la vilabu bingwa hatarini,na hivyobasi kuanzisha mjadala wa iwapo Pep Gurdiola anaweza kuvunja mkataba.

Lakini BBC imebaini kwamba hakuna sheria katika mkataba huo ambao unaweza kumpatia njia ya kuvunja mkataba Guardiola ambaye atajiunga na kilabu hiyo mwezi Julai kama ilivyopangwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha Pep Guardiola

Kushindwa kwa timu hiyo siku ya jumapili kunamaanisha kwamba timu hiyo iko nafasi ya nne na hivyobasi inaweza kufuzu kwa michuano ya vilabu bingwa ikiwa pointi moja juu ya West Ham na Manchester United.

Timu zote zimecheza mechi 30 za ligi ya Uingereza.

Aliyekuwa mkufunzi wa Barcelona Pep Guardiola hajawahi kuifunza timu yoyote katika ligi ya Europa.