Wafuasi wa Besigye wakabiliana na polisi

Image caption wakili wa Besigye

Maafisa wa polisi nchini Uganda wamekabiliana na wafuasi wa upinzani mapema siku ya Jumanne baada ya kutotolewa kwa uamuzi kuhusu kuzuiliwa nyumbani kwa kiongozi wa upinzani Kizza Besigye.

Wafuasi wa Bw Besigye walikongamana nje ya mahakama karibu na Kasangati huko Kampala mapema leo.

Image caption Maafisa wa usalama wasambazwa kukabiliana na wafuasi wa upinzani

Walitarajia kutolewa kwa uamuzi huo katika kesi iliowasilishwa na mawakili wake kufuatia ombi la mkurugenzi wa mashtaka.

Nje ya mahakama wakili wa Besigye David Mpanga alisema kuwa kasi ya vile faili ya kesi hiyo ilivyorudishwa inatia wasiwasi.

Image caption Maafisa wa polisi wakikabiliana na wafuasi wa upinzani nchini Uganda

Wafuasi waliapa kuelekea hadi katika nyumba ya Besgye kabla ya polisi kupelekwa.