Teksi ya Uber yachomwa moto Nairobi

Mtambo wa Uber Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Madereva waTeksi za kawaida Nairobi wanasema Uber inawadhulumu malipo kwa kutumia mitambo ya kisasa ya kielekroniki kuwatoza wateja nauli

Dereva wa teksi ya kampuni ya Uber jana usiku aliteketezwa kwa moto katika mzozo wa unaoendelea baina ya maderevawa teksi za kawaida na zile zinazotumia teknolojia ya kisasa kuwatoza wateja wao nauli katika mji mkuu wa kenya-Nairobi.

Polisi wanasema kuwa gari hilo la Uber lilichomwa moto katika kitongoji cha Riruta jijini Nairobi na watu wanne waliokua wakilisubiri, lakini hata hivyo dereva alinusurika kuchomwa, limeripoti gazeti la Daily Nation.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Si mara ya kwanza kwa mashambulio dhidi ya magari ya kampuni ya Uber kushambuliwa mjini Nairobi

"wanne hao waliungana na mwanamume mwingine mmoja ambae alikodisha teksi hiyo na dereva aliruka kutoka ndani na kutimua mbio ," Alisema mkuu wa polisi jijini Nairobi Japheth Koome.

Hili ni tukio la pili la aina hii katika kipindi cha mwezi mmoja katika jiji la Nairobi.

Mwezi Februari, madereva teksi za kawaida walifanya maandamano jijini Nairobi na walipatia kampuni ya Uber siku saba iwe imesitisha shughuli zake nchini Kenya,baada ya kuishutumu kuvunja sheria za nchi na kuhusika kuwa na ukoloni mamboleo.