Brussels: Salah Abdeslam kwenda Ufaransa

Haki miliki ya picha PN Belggique
Image caption Mshukiwa mkuu wa mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Paris Ufaransa

Wakili wa mshukiwa mkuu wa mashambulio ya mabomu katika mji mkuu wa Paris Ufaransa mwezi Novemba mwaka jana,Salah Abdeslam,anasema kuwa hatapinga kuhamishwa kwa mteja wake hadi Ufaransa.

Salah Abdeslam, alikamatwa na polisi juma lililopita nchini Ubelgiji kufuatia operesheni ya kufamania.

Wakili huyo Sven Mary, anasema kwamba mteja wake amemwambia kuwa hakuelewa mapema kuhusiana na mipango ya mashambulio yaliyotokea Ubelgiji.

Watu 31 waliuawa baada ya mashambulio ya mabomu ya kujitolea muhanga yaliyotokea kwenye uwanja wa ndege na reli ya chini kwa chini mjini Brussels siku ya Jumanne.

Image caption Wakili Sven Mary

Islamic State (IS) imedai kutekeleza mashambulizi hayo.

Wakili Mary amesema kuwa Abdesalam mwenye umri wa miaka 26 mzaliwa wa Ubelgiji ameomba apelekwa mara moja nchini Ufransa iliajieleze.

Wakili huyo awali alikuwa amesema kuwa atapinga kuhamishwa kwake hadi Ufaransa ilikujibu mashtaka dhidi yake.

Haki miliki ya picha VTM via AP
Image caption Salah Abdeslam, alipokamatwa na polisi juma lililopita nchini Ubelgiji

Mawaziri wawili wa Ubelgiji walikuwa wamejiuzulu kufuatia mashambulizi hayo baada ya kubaini kuwa walipuuza ushauri wa Uturuki kuwa mmoja wa magaidi aliyejilipua alikuwa ameshapata mafunzo yenye itikadi kali aliporejeshwa kwao kwa nguvu.

Waziri wa usalama wa ndani Jan Jambon na mwenzake wa Sheria Koen Geens, waliomba wajiondoe lakini maombi yao yakakataliwa.

Waziri mkuu wa Ubelgiji bwana Charles Michel hata hivyo amekataa kukubali maombi yao.

Uturuki ilisema kuwa iliionya Brussels kuhusiana na Brahim el-Bakraoui lakini ikapuuzwa.