Sassou Nguesso ashinda tena urais Congo

 Denis Sassou-Nguesso Haki miliki ya picha
Image caption Rais wa Denis Sassou-Nguesso amekua malakani kwa zaidi ya miaka 30

Rais wa Congo- Brazaville, Denis Sassou-Nguesso, ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais, ambao upinzani umeupinga kwamba ulikumbwa na wizi wa kura.

Akizungumza katika televisheni ya taifa, waziri wa mambo ya ndani nchini humo Raymond Zephyrin Mboulou amesema kwamba Bwana Sassou Nguesso - ambaye amekua mamlakani kwa zaidi ya miaka thelathini amezinyakulia zaidi ya asilimia sitini ya kura.

Image caption Rais Denis Sassou-Nguesso alishinda kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba

Taarifa rasmi zinasema mpinzani wake wa karibu Guy-Brice Parfait Kolelas, na generali mstaafu Jean-Marie Mokoko wako nyuma wakiwa na asilinia kumi na tano na kumi na nne ya kura. Wamesema hapa kulikua na "wizi mkubwa" na kutoa wito kura zihesabiwe upya.

Bwana Sassou-Nguesso alishinda kuidhinishwa kwa mabadiliko ya katiba mwaka jana ili kumruhusu agombee tena kwa muhula mwingine wa miaka 7 zaidi mamlakani.