Muisraeli aliyeuwa mpalestina akamatwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Muisraeli aliyeuwa mpalestina akamatwa

Mwanjeshi Muisraeli amekamatwa baada ya video kufichuliwa inayomuonesha akimpiga risasi na kumuua mpalestina aliyekuwa amesalimu amri.

Katika video hiyo afisa huyo wa usalama anaonekana akimpiga risasi kichwani mtu aliyelala chini katika mji wa Hebron.

Mpalestina huyo tayari alikuwa amejeruhiwa.

Muda mchache baadaye alimtangaza mpalestina huyo kuwa amefariki dunia.

Image caption Idara ya ulinzi ya Israeli ilikiri kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina.

Makundi ya kupigania haki za kibinadamu ndiyo yaliyochapisha video hiyo.

Idara ya ulinzi ya Israeli ilikiri kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kufanya uchunguzi wa kina.