Kuna matumaini ya hatma ya ndege ya Malaysia iliyotoweka

Kifusi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kifusi cha ndege kilichopatikana nchini Msumbiji kinachoaminiwa kuwa cha ndege ya Malasyia iliyotoweka

Waziri wa uchukuzi wa Australia anasema kwamba vifusi vya ndege mbili vilivyopatikana nchini Msumbiji "vinaelekea kuwa kama " vilitoka kwenye ndege iliyotoweka ya Malaysia chapa MH370.

Vifusi viwili vilipatikana katika maeneo tofauti na wananchi na vilisafirishwa hadi nchini Australia kwa uchunguzi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jamaa wa waathiriwa 239 waliokuwame ndani ya ndege bado hawajui hatma ya ndugu zao hadi leo

Darren Chester amesema kuwa matokeo ya uchunguzi "yalikuwa ya kuimarika na vilifanana na ya kushangaza" kuhusu namna vifusi hivyo kutoka ndege iliyotoweka viliweza kusafirishwa na mawimbi ya bahari. MH370 ilipotea mwezi Machi 2014 ikiwa na watu 239 ndani.

Ilipotea katika mawasiliano ilipokua angani kutoka mji mkuu wa Malaysia Kuala Lumpur kuelekea Beijing na inaaminiwa kwa kiasi kikubwa kwamba ilianguka katika bahari ya Hindi baada kutokana na sababu bado hazijafahamika.

Hatma ya ndege hiyo , abiria wake na wahudumu imebakiwa isiyojulikana.