Imam wa Glasgow ampongeza muuaji

Image caption Imam Maulana

Kiongozi wa dini katika msikiti mkubwa wa Glasgow nchini Uskochi amempongeza mtu mmoja mwenye itikadi kali ambaye alinyongwa kwa kutekeleza mauaji nchini Pakistan.

Imam Maulana Habib Ur Rehman wa msikiti wa katikati mjini Glasgow alitumia mtandao wa WhatsApp kumuunga mkono Mumtaz Qadri.

Qadri alinyongwa mnamo mwezi Februari baada ya kumuua mwanasiasa mmoja ambaye alipinga sheria kali ya kufuru.

Katika taarifa Imam huyo alisema kuwa ujumbe huo ulieleweka vibaya.

Alisema kuwa alikuwa anatoa maoni yake yanayopinga watu kunyongwa.

Katika Ujumbe ulioonekana na BBC ,imam Maulana Habib Ur Rehman anasema ''amekasirishwa'' na ''kusumbuliwa'' kuhusu habari za kunyongwa kwa Qadri,na baadaye kuandika ''rahmatullahi alai'' ikiwa ni baraka za kidini zinazopewa mtu anayefuata dini.

Katika ujumbe mwengine anasema ''siwezi kuficha uchungu wangu leo''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mumtaz Qadri

Mwislamu wa haki aliadhibiwa kwa kufanya kile amacho taifa zima lilishindwa kukifanya.

Qadri aliajiriwa kama mlinzi wa gavana wa mkoa wa Punjab nchini Pakistan Salman Taseer kabla ya kumgeukia mwaka 2011 na kumpiga risasi mara tisa.

Baada ya kumpiga risasi Qadri alidaiwa kuwaambia waandishi kwamba anafurahia alichofanya na kwamba amemaliza ''kufuru''.