Korea Kaskazini yafanya zoezi la kushambulia makao ya rais

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Makao ya rais wa Korea Kusini Park Guen-Hye

Korea Kaskazini imesema kuwa imetekeleza mazoezi ya kuyashambulia makaazi ya rais wa Korea Kusini.

Zoezi hilo lilisimamiwa na rais wa taifa hilo Kim Jong-un,kulingana na chombo cha habari cha KCNA ambaye alilitaka jeshi kujiandaaa kuivamia na kuiharibu serikali ya kusini.

Ni hatua ya hivi karibuni ya ishara za hasira za Pyongyang.

Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye ameliagiza jeshi lake kuwa katika hali ya tahadhari.

Lakini alisema siku ya Alhamisi kwamba uchochezi utasababisha maafa makubwa kwa serikali na uongozi wa Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong-un

Korea Kaskazini imekuwa ikijibu hatua ya Umoja wa Mataifa ya kuiwekea vikwazo kufuatia majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ya kinyuklia.

Pyongyang vile vile imekasirishwa na mazoezi ya pamoja kati ya serikali ya Korea Kusini na Marekani kusini mwa mpaka wake.

Kama inavyojulikana kwa vitisho vyake ,ripoti hiyo iliotolewa na KCNA ilitishia kuilipua nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini inayojuliakana kama Blue House hadi kuwa jivu.

Makombora yalirushwa kama umeme na kuanguka katika maeneo yanayolengwa ikiwemo nyumba hiyo ya rais wa Korea Kusini.

Haijulikani ni lini zoezi hilo lilifanywa,lakini ripoti hiyo ilionya mwisho mbaya wa rais Park.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Korea Kusini Park Geun Hye

Makaazi hayo ya Blue House yalishambuliwa na makomando wa Korea Kaskazini mwaka 1968.

Hatahivyo jaribio la kutaka kumuua aliyekuwa rais Park Chung-hee halikufanikiwa,raia saba wa Korea Kusini pamoja na makomando hao 31 kutoka Korea Kaskazini waliuawa.