Akamatwa kwa kuipelelezea Korea Kusini

Image caption Kim Dong Chul

Raia wa Marekani aliyekamatwa nchini Korea Kaskazini amesema kuwa aliiba siri za kijeshi za Korea kaskazini ili kuisaidia Korea Kusini katika taarifa na waandishi wa habari ilioandaliwa na Pyongyang.

Kim Dong Chul mwenye umri wa miaka 62 alikiri kufanya hivyo siku ya ijumaa,akiomba msamaha kwa kupeleleza.

Bwana Kim awali aliwaambia waandishi kwamba yeye ni raia wa Marekani aliyezaliwa nchini Korea Kusini na kwamba alikamatwa mwezi Oktoba kwa kufanya upelelezi.

Image caption Kim Dong Chul

Bwana Kim amesema kwamba alikutakana na maafisa wa upelelezi kutoka Korea Kusini mwaka 2011 ili kuifanyia uchunguzi,kulingana na shirika la habari la KCNA kutoka nchini Korea Kaskazini.

Alikamatwa wakati alipokuwa akichukua habari za kijasusi za kijeshi na zile za kinyuklia kutoka kwa mtu ambaye hakutajwa.