Walioshambulia Ufaransa na Brussels kuangamizwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maafisa wa polisi nchini Ubelgiji

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa kundi la Waislamu wenye itikadi kali walioshambulia Ufaransa mwaka uliopita na mashambulizi ya juma lililopita ya Brussels wanaendelea kuangamizwa.

Alisema Serikali za Ufaransa na Ubelgiji zimefaulu kupata wanakojificha wengi wa wapiganaji hao na kuwatia mbaroni.

Hata hivyo, Rais Hollande, alisema kundi hilo bado ni tishio kwa wakaazi wa Ulaya.

Haki miliki ya picha Belgian police
Image caption Washukiwa wa mlipuko katika uwanja wa ndege

Maafisa wa polisi wa Ubelgiji wamewapiga risasi na kuwajeruhi washukiwa wawili katika oparesheni ya hivi karibuni.

Picha za video zinaonyesha maafisa wa usalama waliojihami na kujifunika kikamilifu wakiwa wamemlenga mwanamume mmoja aliyekuwa amejeruhiwa kabla ya kumkokota kwa miguu yake.