Wafanyibiashara 250 wataka UK ijiondoe EU

Image caption Bendera ya UIngereza na ile ya muungano wa Ulaya

Orodha ya wafanyibiashara 250 wanaoiunga mkono Uingereza kujiondoa katika muungano wa Ulaya imechapishwa na kundi la wale wanaounga mkono kujiondoa.

Orodha hiyo inashirikisha mkurugenzi mkuu wa HSBC Michael Geogheghan,mwanzilishi wa Phones 4u John Caudwell pamoja na mfamyibiashara wa hoteli Rocco Forte.

Lakini wale wanaounga mkono Uingereza kusalia katika muungano huo wanasema kuwa wale wanaotaka Uingereza kujiondoa hawakuweza kupata wafanyibiashara wa kuunga mkono kura yao kwa kuwa wale walioorodheshwa wanaunga mkono kura hiyo kibinafsi.

Kura ya maoni kuhusu iwapo Uingereza itasalia katika muungano huo itafanyika mwezi Juni 23.

Mwezi uliopita,wakuu wa kampuni 36 zilizoorodheshwa nchini Uingereza kuwa kubwa walitia sahihi barua ya kuwataka wapiga kura kusalia katika muungano wa Ulaya.

Lakini Matthew Elliot,ambaye ni mkuu wa wale wanaotaka Uingereza kujiondoa EU amesema kuwa wana orodha kubwa ya wafanyibiashara wanaowaunga mkono.