Fujo lazuka katika ukumbusho Brussels

Haki miliki ya picha AP
Image caption Fujo lazuka katika ukumbusho Brussels

Polisi wa kupambana na fujo wamekabiliana na waandamanaji wazungu wanaopinga kuwepo kwa watu wenye rangi tofauti nchini Ubelgiliji katika medani ya umma iliyokuwa inatumiwa kutoa heshima za mwisho kwa wahanga wa shambulizi la kigaidi lilitokea mjini Brussels mapema juma lililopita.

Kundi hilo la Mafashisti liliingia kwa nguvu kwenye medani ilioko katikati ya mji, ilioko mbele ya soko la hisa.

Waliwakabili wanawake WaIslamu waliokuwako hapo kwenye medani hiyo.

Haki miliki ya picha PATRIK STOLLARZ AFP Getty Images
Image caption Polisi walilazimika kutumia mabomba ya maji kuwarudisha nyuma.

Watu hao waliokuwa wamevalia mavazi meusi walipiga saluti za KiNazi, na walipiga kelele kwa muda mfupi, kabla ya polisi kuingilia kati na kurejesha utulivu.

Polisi walilazimika kutumia mabomba ya maji kuwarudisha nyuma.

Kumi kati yao walikamatwa na polisi.

Mapema leo, polisi nchini Ubelgiji waliendelea kufanya misako sehemu mbalimbali za nchi kuwatafuta washambuliaji.

Taarifa ya ofisi ya mkuu wa mashtaka nchini humo, ilieleza kuwa watu 9 wamekamatwa, na wanne bado wanasailiwa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kumi kati yao walikamatwa na polisi.

Wakati huohuo, maafisa wa uwanja wa ndege wa Brussels wanasema polisi wamemaliza uchunguzi wao , baada ya mashambulio ya kujitolea mhanga yaliyofanywa juma lilopita.

Ukaguzi wa jumba la uwanja wa ndege, unaonesha kuwa jengo lenyewe ni imara na linaweza kufunguliwa kwa umma.