Brussels: Aliyeghushi vyeti vya usafiri anaswa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Brussels: Aliyeghushi vyeti vya usafiri anaswa

Polisi wa Italia wamemkamata mwanamume mmoja kutoka Algeria, ambaye anashukiwa kughushi vitambulisho vya bandia, ambavyo vilitumiwa na washambuliaji wa mjini Paris na Brussels.

Djamal Eddine Ouali, mwenye umri wa miaka 40, alikamatwa kufuatana na amri ya Umoja wa Ulaya, karibu na Salerno, kusini mwa Utaliana.

Ripoti zinasema kuwa jina lake lilipatikana kwenye nyaraka, zilizopatikana wakati nyumba moja ya mjini Brussels, ilipovamiwa mwezi wa Oktoba mwaka jana.

Haki miliki ya picha Belgian Federal Police
Image caption Djamal Eddine Ouali, mwenye umri wa miaka 40, alikamatwa kufuatana na amri ya Umoja wa Ulaya

Jina la bwana huyo pamoja na picha za wapiganaji, ambao baadaye walifanya mashambulio mjini Paris na Brussels.