Fujo lazuka Guinea B. ilipoilaza Kenya 1-0

Image caption Fujo lazuka Guinea B. ilipoilaza Kenya 1-0

Guinea Bissau iliichapa Harambee stars ya Kenya bao 1-0 nyumbani kwao katika mechi ya marudiano ya kufuzu kwa fainali ya kombe la mataifa ya Afrika yatakayoandaliwa Gabon mwakani.

Guinea Bissau ilitumia vyema nafasi iliyoipata licha ya maelfu ya mashabiki wa Stars kuishangilia timu yao katika uwanja wa Nyayo mjini Nairobi mapema leo.

Kufuatia ushindi huo, Guinea Bissau sasa imejikita kileleni mwa kundi E baada ya kuilaza Kenya nyumbani na ugenini.

Kenya kwa upande wao wamesalia katika nafasi ya mwisho na watajilaumu wenyewe kwa bao hilo la Mendes dakka tisa kabla ya kipenga cha mwisho.

Hata hivyo bao hilo liliwaudhi sana mashabiki wa Harambee Stars ambao walihisi mpira haukuwa umevuka laini.

Kwa hasira walipura mawe na chupa uwanjani na kumlazimisha refarii kusimamisha mechi hiyo kwa muda wa nusu saa hivi.

Polisi walilazimika kutupa mabomu ya kutoa machozi ilikuwatawanya mashabiki waliojawa na hasira.

Kufuatia machafuko hayo haijabainika shirikisho la soka Afrika CAF litaichukulia Kenya hatua gani.

Matokeo Mengine

Msumbiji 0-0 Ghana

Kenya 0-1 Guinea-Bissau

Congo 1-1 Zambia

Botswana 2-1 Comoros

Benin 4-1 Sudan Kusini