Polisi Pakistani wakabiliana na waandamanaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waandamanaji wafuasi wa Mumtaz Qadri

Polisi nchini Pakistani wamekabiliana na waaandamanaji kwa kuwafyatulia mabomu ya kutoa machozi katika mji mkuu wa Islamabad ambao walikuwa wakiandamana kupinga hatua ya mpiganaji wa kiislamu kunyongwa.

Qadri alinyongwa mwezi uliopita baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya gavana wa Punjap Salman Taseer aliyoyafanya miaka mitano iliiyopita. Bwana Taseer alikuwa alikuwa akimtetea mwanamke wa kikristo aliyefungwa jela kutoka na makosa ya kukufuru. Wafuasi wa Mumtaz Qadri wanamuona muuaji huyo kama shujaa wa kidini.