Afisa wa chanjo ya Polio Pakistan auawa

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Afisa wa kutoa chanjo ya Polio Pakistan auawa

Afisa wa idara ya afya nchini Pakistan aliyekuwa akisimamia kampeini ya kutoa chanjo ya kupambana na maradhi ya polio maeneoya vijijini karibu na mpaka na Afghanistan ameuawa kwa kupigwa risasi.

Bwana Akhtar Khan alikuwa katika zahanati yake ya afya wakati aliposhambuliwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kutokana na vitendo kama hivyo imekuwa vigumu kutokomeza maradhi ya polio

Baadhi na wanamgambo na wapiganaji katika maeneo hayo wanadai kuwa dawa hiyo ya chanjo inauiwa kuwafanya watoto kutoka jamii hiyo wasiwe na uwezo wa kuzaa watakapokuwa wametimiza umri.

Kutokana na vitendo kama hivyo imekuwa vigumu kutokomeza maradhi ya polio katika mataifa hayo mawili ya Pakistan na Afghanistan .