Assad asifu jeshi kwa kuikomboa Palmyra

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Assad asifu jeshi kwa kuukomboa Palmyra

Rais wa Syria, Bashar al-Assad, amesifu mafanikio makubwa ya jeshi lake ya kuukomboa kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State, mji wa Palmyra.

Rais Assad alisema huo ni ushahidi wa hivi punde, juu ya ufanisi wa jeshi la Syria na washirika wake wanaopigana na ugaidi (Urusi).

Haki miliki ya picha REUTERS SANA
Image caption Rais Assad alisema huo ni ushahidi wa hivi punde, juu ya ufanisi wa jeshi la Syria na washirika wake

Ndege za kijeshi za Urusi zilichangia sana katika mashambulio ya majuma matatu, ya kuwatoa IS katika mji huo, ambao ulitekwa mwezi Mei mwaka jana.

Syria imekumbwa na vita kwa miaka 5 sasa
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mji huo ulioko jangwani ni mji maarufu kwa magofu yake ya kale.

Wakati Palmyra ikidhibitiwa na IS, magofu yake yalibomolewa kusudi na wanamgambo hao jambo lilolaaniwa na jamii ya kimataifa.

Majeshi ya serikali ya Syria yamekuwa yakipiga hatua kuteka maeneo yanayokaliwa na wapinzani wao na vilevile yaliyokuwa yametekwa na IS tangu majeshi ya Urusi yalipoingia Syira kuisaidia serikali ya Bashar al Asaad kwa mashambulizi makali ya angani .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Majeshi ya serikali ya Syria yamekuwa yakipiga hatua na kuteka maeneo yanayokaliwa na wapinzani kwa msaada wa ndege za Urusi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights limesema bado kuna milio ya ufyatulianaji risasi upande wa mashariki mwa mji huo lakini wengi wa wapiganaji wa IS wamefurushwa na kulazimika kurudi nyuma.