FIFA: Aliyekuwa rais wa Honduras alipokea hongo

Haki miliki ya picha f
Image caption Aliyekuwa rais wa Honduras, Rafael Callejas, amekiri kushiriki ufisadi

Aliyekuwa rais wa Honduras, Rafael Callejas, amekiri kushiriki ufisadi na kwa kupokea hongo kuhusiana na tuhuma zilizotolewa dhidi ya maafisa wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Rais huyo wa zamani Callejas, alikubali makosa mawili ya kupokea hongo na kushiriki ufisadi.

Bwana Callejas alipokea hongo hiyo akiwa rais wa shirikisho la soka la Honduras.

Alikiri makosa hayo mbele ya mahakama mjini New York Marekani.

Rais huyo wa zamani ni miongoni mwa maafisa 42 na mashirikisho yaliyonaswa na mtego wa kiongozi wa mashtaka kutoka Marekani aliyekuwa akiendesha uchunguzi dhidi ya maafisa wa FIFA wafisadi aliodai walipokea takriban dola mia mbili milioni pesa za Marekani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Alikiri makosa hayo mbele ya mahakama mjini New York Marekani.

Uchunguzi huo ililenga kuthibitisha kuwa kandarasi za uwenyeji na hati mili ya kupeperusha mecho za kombe la dunia zilikuwa zikitolewa tu kwa mashirika na watu walokuwa wakitoa mlungula.

Kufuatia kukiri kwa bwana Callejas sasa mahakama hiyo inatarajiwa kutoa hukumu yake ambapo anakabiliwa na hadi miaka 20 gerezani.